Top news
MEJA JENERALI MABELE ATEMBELEA BANDA LA JKT KWENYE MAONESHO YA SABASABA DAR
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ametembelea Banda la JKT katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yaliyozinduliwa leo Julai 3,2024 katika viwanja vya Mwl.JK Nyerere Barabara ya Kilwa Mkoani Dar es Salaam.
Meja Jenerali Rajabu Mabele ameongozana na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata.
Wakiwa katika Banda hilo wamepata maelezo ya namna JKT linavyozalisha Mali kupitia Vikosi, Makambi, Shule na Kampuni Tanzu za Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT).
Frank Jordan
12345
123
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

