CGP NYAMKA AWAVISHA VYEO ASKARI 27 WA JESHI LA MAGEREZA
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka leo tarehe 28.6.2023 amewavisha cheo askari 27 wa Makao Makuu kutoka cheo cha Sajenti ( SGT) kuwa Staff Sajenti (S'SGT) katika Ukumbi wa Meja Jenerali Suleiman Mzee uliopo Makao Makuu ya Magereza eneo la Msalato Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuwavisha cheo askari hao,CGP Nyamka pamoja na Mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu katika maeneo ya kazi,ili kuleta tija kwa Jeshi na Taifa kwa ujumla.
"Kupandishwa cheo sio kupunguziwa majukumu ni kuongezewa majukumu" alisema Nyamka.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Jeshi, Kaimu Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu DCP.Jeremiah Katungu amemshukuru Kamishna Jenerali kukubali kupandishwa na kuwavalisha vyeo askari hao,huku akiwapongeza wahusika wote.
Jumla ya askari 667 wamepandishwa cheo nchi nzima.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news