logo

TANZANIA KUPATA UZOEFU UZALISHAJI MAFUTA YA MAWESE NCHINI INDONESIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kwa kuwa nchi ya Indonesia ni mzalishaji mkubwa wa mafuta ya mawese duniani, amemueleza Rais Widodo kuhusu nia ya Tanzania kupata uzoefu wa nchi yake katika uzalishaji wa mafuta hayo na hivyo kufufua sekta husika.

.

Rais Samia ameyasema hayo leo Agosti 22,2023 wakati wa ziara ya Rais wa Indonesia mhe.Joko Widodo nchini Tanzania.

.

Amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana kukuza biashara na uwekezaji kwa kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi.

.

"tumedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano wetu katika viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi, uvuvi, utalii na sekta za ukarimu na kubadilishana maarifa na teknolojia" amesema Rais Samia.

.

Rais Samia pia amemuomba Rais Widodo ushirikiano zaidi katika kujenga uwezo na ujuzi wa kiufundi kwenye mageuzi ya sekta ya kilimo, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maendeleo makubwa ya miundombinu nchini, uendeshaji wenye tija na ufanisi wa mashirika ya kibiashara yanayomilikiwa na serikali.

.

Aidha, kuhusu uchumi wa buluu uliopewa kipaumbele cha kwanza Zanzibar, Rais Samia amemuomba Mhe.Widodo kushirikiana pamoja hususani kwenye sekta hiyo na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa kwenye ujenzi wa bandari kubwa itakayotoa huduma mbalimbali zinazohusu uchumi wa buluu.

.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mhe.Joko Widodo amesema Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mhe.Soekarno.

"Indonesia imekuwa ikitoa fursa za ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwenye fani mbalimbali katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Nakukaribisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutembelea nchi ya Indonesia" amesema Rais huyo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn