logo

PROF.KABUDI:MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAIMARIKA TANZANIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba J.A. Kabudi (Mb), amewasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya nchini ya Mwaka 2025.

‎Taarifa hiyo imebainisha hatua mbalimbali zilizofikiwa na Serikali katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya, kuimarisha huduma za tiba na utengamao kwa watu wenye uraibu, pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

‎Akizungumza na waandishi wa habari Bungeni jijini Dodoma leo baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Prof. Kabudi amesema uwasilishaji wa taarifa hiyo ni utekelezaji wa Kifungu cha 66 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015, kinachoitaka Serikali kuandaa na kuwasilisha Bungeni taarifa hiyo kila mwaka kwa lengo la kuonesha uwajibikaji kwa wananchi na kutathmini utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti dawa za kulevya nchini.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn