logo

AYOUB LAKRED ATANGAZWA KUWA GOLIKIPA WA SIMBA SC

Klabu ya Simba imemtangaza golikipa wa kimataifa wa Morocco Ayoub Lakred kuwa nyanda wao mwingine.

Ni katika mji wa Bouznika, mji wenye fukwe nzuri zaidi nchini Morocco za bahari ya Atlantic na kitovu cha utalii wa fukwe na historia uliopo pembeni ya Casablanca kaskazini magharibi mwa Morocco mnamo 21/06/1995 ndipo alipozaliwa golikipa Ayoub Lakred.

Ni golikipa anayemudu zaidi kupiga mpira kwa mguu wa kulia na uwezo mzuri wa kupiga pasi ndefu akiwa na umbo kubwa (Bonge la mtu) na urefu wa futi 6 na nchi 1 na uzito wa Kilogram 87.

Mechi 129 amefunga goli 1 na kuokoa penati 6 na mechi yake ya mwisho kucheza ni Juni 23 mwaka huu dhidi ya Ittihad Tanger.

Alianza kucheza mpira angali mdogo akiwa kwenye timu za mitaani na alikuwa akicheza kama beki au winga lakini maisha yakampeleka golini.

Baada ya kukamua ndondo za kutosha ilikuwa bahati kwake kuonwa na timu ya vijana ya RS Berkane na mnamo July 2014 akapandishwa timu ya wakubwa.

Alikumbana na upinzani wa namba kwa makipa wazoefu Mounir Lemrabet aliyecheza mechi 23 na Ahmed Reda Tagnaout aliyecheza mechi 7 huku yeye akidaka mechi 1 pekee!

Aliendelea kujituma na kupata nafasi kikosini mara kadhaa ingali hakuingia kwenye kikosi cha kwanza na kwenye dirisha kubwa la usajili la 2019 alifanikiwa kuhamia kwenye klabu ya Association sportive des Forces armées royales yaani AS FAR.

Huko aliingia taratibu kikosini na baada ya mkataba wake kumalizika 2021 aliongeza mkataba mwingine kusalia klabuni na msimu uliopita aliiongoza AS FAR kutwaa ubingwa wa Ligi ya Morocco!

Ana uwezo mzuri wa kucheza krosi na mipira ya 1 v 1 pia kwenye mipira ya hewani ni mzuri sana. Ana udhaifu kiasi kwenye mipira ya chini.

Ni kipa aliyejumuishwa kwenye timu ya Taifa ya Morocco ya CHAN mara kadhaa! Simba wamepata kipa mzuri otherwise mazingira yamkatae.

Vilio sasa basiee!?.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn