FORBES YATOA ORODHA YA TOP 10 YA WANAWAKE MATAJIRI ZAIDI MAREKANI
JARIDA la Forbes limetoa Orodha ya Mwaka huu 2023 ya Wanawake Matajiri Zaidi 10 Ambao ni Maarufu waliojitengeneza Utajiri Wao Kupitia Biashara, Mali au Vitu Mbalimbali wanavyovimiliki.
.
Ifuatayo Ni Orodha Kamili ya Wanawake hao 10 wanaoongoza Kuwa Na Utajiri Zaidi;
.
Wa Kwanza, Oprah Winfrey ni mjasiriamali wa Media, mwigizaji, mtayarishaji. Winfrey anajulikana zaidi kwa kipindi chake cha Runinga anachoongea na wageni wake kinachojulikana kama 'Oprah Winfrey Show' chenye watazamaji wengi, Na ana Utajiri wa Dola Bilioni 2.5 za Kimarekani.
.
Wa Pili, Ni Mwanamuziki, Mjasiriamali na Mfanyabiashara Maarufu Rihanna ambaye Utajiri wake Ni Dola Bilioni 1.4 za Kimarekani.
.
Wa Tatu, Ni Kim Kardashian Ambaye mwanamitindo, na mfanyabiashara wa Kimarekani, Ana Utajiri Wa Dola Bilioni 1.2 za Kimarekani.
.
Wa Nne, Taylor Swift Ni Mwimbaji na Mtunzi wa Muziki wa Country-Pop nchini Marekani na ana Utajiri wa Dola Milioni 740 za Kimarekani.
.
Wa Tano, Ni Mwanamitindo Na Mfanyabiashara Kylie Jenner ambaye ana Utajiri wa Dola Milioni 680 za Kimarekani.
.
Wa Sita, Ni Mwanamuziki Madonna ambaye ana Utajiri wa Dola Milioni 580 za Kimarekani.
.
Wa Saba, Ni Beyonce Ana Utajiri Wa Dola Milioni 540 za Kimarekani.
.
Wa Nane, Ni Celine Dion ambaye ana Utajiri wa Dola Milioni 480.
.
Wa Tisa, Ni Judy Sheindlin ambaye Ni Jaji wa Mahakama Na ana onyesho lake maarufu la mahakama la Mchana ambalo lilimletea mamilioni na Utajiri wake ni Dola Milioni 480 za Kimarekani.
.
Na wa Kumi Ni Dolly Parton ambaye Utajiri wake Ni Dola Milioni 440.Huyu amekuwa akishughulika na vipindi maalum vya televisheni, vitabu vipya na laini mpya za bidhaa mwaka uliopita
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

