logo

NEMC YAINGIA MKATABA NA WASANII WA MUZIKI-UBALOZI WA MAZINGIRA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeingia mkataba wa ushirikiano na wasanii wa muziki Mzee Yusuph, Mrisho Mpoto na MYCOELY kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira kupitia nguvu ya sanaa na muziki.

‎Kupitia ushirikiano huo, wasanii hao watatumika kama Mabalozi wa Mazingira, wakifikisha ujumbe wa utunzaji wa mazingira, usimamizi sahihi wa taka, upandaji miti na matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira kwa makundi mbalimbali ya wananchi nchini.

‎Hatua hii inaonesha dhamira ya NEMC ya kutumia mbinu bunifu katika kuelimisha umma, kwa kuunganisha nguvu ya wasanii wenye ushawishi mkubwa ili kuongeza uelewa na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn