logo

RAIS SAMIA KUZINDUA MRADI MKUBWA WA MAFUTA KIGAMBONI JIJINI DAR

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kesho tarehe 3 March 2026, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa matenki 15 ya kuhifadhia mafuta yenye thamani ya Sh bilioni 678.6 katika eneo la Kigamboni Mnadani, Jijini Dar es Salaam.

‎Akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es salaam tarehe 02 Machi, 2026 Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema mradi huo ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam unaolenga kuongeza ufanisi, ushindani na mchango wake katika uchumi wa taifa.

‎Amesema matenki hayo yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 378,000 za mafuta na yatapunguza muda wa meli za mafuta kukaa bandarini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku 3, hatua itakayoongeza ufanisi, kuvutia wawekezaji na kuimarisha usalama wa nishati.

Prof. Mbarawa ameongeza kuwa mradi huo unaenda sambamba na ujenzi wa magati mapya yenye urefu wa mita 500 kila moja, yakitarajiwa kuongeza uwezo wa bandari Mpaka kufikia kuhudumia tani milioni 60 kwa mwaka.

‎Amesema Katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, Bandari ya Dar es Salaam ilihudumia tani milioni 19.9 za mizigo, huku Serikali ikilenga kufikia tani milioni 40 ifikapo mwaka wa fedha 2025/26.

‎Aidha, amesema maboresho hayo yanaendana na mkakati wa kuimarisha usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR), ili kupunguza utegemezi wa barabara na kuongeza ufanisi wa usafirishaji ndani na nje ya nchi.

‎Waziri Mbarawa ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es salaam na viunga vyake na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo kubwa na la kihistoria kwa nchi yetu.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn