logo

WANAFUNZI WACHUANA KUONESHA UMAHIRI KATIKA UHANDISI MITAMBO NA USANIFU WA KIHANDISI

Mashindano ya Ujuzi Kitaifa 2026 yanaendelea kufanyika nchini, ambapo tarehe 9 Juni, 2026 wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walishiriki mchujo katika eneo la Uhandisi Mitambo na Usanifu wa Kihandisi kwa kutumia Kompyuta ngazi ya Kanda uliofanyika katika chuo Ufundi Arusha (ATC), mkoani Arusha.

‎Washiriki walichuana umahiri wao katika kubuni, kuchambua na kutatua changamoto za kiufundi kwa kutumia teknolojia za kisasa za usanifu wa kompyuta.

‎Mashindano ya Kitaifa ya Ujuzi, yalianza tarehe 8 Juni 2026 na yanalenga kuhamasisha maendeleo ya ujuzi miongoni mwa vijana kupitia elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, ili kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira n akucnagia maendeleo ya uchumi wa taifa.

‎Washindi ngazi ya kanda watapata fursa ya kushiriki ngazi ya Taifa Mwezi Agosti, 2026, ambapo washindi watapata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Ujuzi ya Afrika.

‎Mashindano haya yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na ni ya

‎kwanza kufanyika tangu Tanzania ijiunge na uanachama wa Worldskills Africa, hatua inayofungua fursa zaidi kwa vijana wa Kitanzania kushiriki na kushindana katika majukwaa ya kimataifa ya maendeleo ya ujuzi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn