logo

WANANCHI 823 WATARAJIWA KUFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO IGUNGA

Jumla ya macho 996 yamefanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa 823 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika kambi maalum ya madaktari bigwa iliyowekwa na Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya 'Helen Keller International' na wadau wengine wa sekta ya afya.

‎Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. Elizabeth Rwegasila amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kambi ya madaktari bingwa wa macho iliyowekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha afya ya macho na kuondoa tatizo la upofu kwa wananchi.

‎"Idadi hii inaonesha ukubwa wa mahitaji ya huduma za macho kwa wananchi wa eneo hili, wanaonufaika na huduma hiyo wanapatiwa huduma mbalimbali muhimu ikiwemo usafiri kutoka majumbani mwao, malazi, chakula pamoja na huduma za matibabu kabla na baada ya upasuaji," amesema Mhe. Rwegasila

‎Aidha, amelishukuru Shirika la Helen Keller International kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya ya macho, akieleza kuwa mbali na kutoa huduma za matibabu, shirika hilo limechangia kuwajengea uwezo wataalamu wa afya ili kuendeleza huduma hizo hata baada ya mradi kukamilika.

‎Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wizara ya Afya Dkt. Greater Mande amesema mtoto wa jicho ni miongoni mwa sababu zinazosababisha upofu kwa wananchi wengi, kupitia kambi hiyo wagonjwa wengi wamepata fursa ya kurejeshewa uwezo wao wa kuona na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

‎Pia, Dkt. Mande amewahimiza wananchi watakaonufaika na huduma hizo kuwa mabalozi kwa jamii zao kwa kutoa taarifa kwa watu wengine wenye changamoto za macho ili waweze kujitokeza kupata matibabu wanapopata fursa hiyo.

‎Nae, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Boniface Marwa amesema wataendelea kushirikiana na wadau ili huduma hiyo ya upasuaji na mtoto wa jicho inakua endelevu na wananchi waendelee kupata huduma hizo pamoja na kuwashukuru Helen Keller kwa kuwasimesha wataalam wa eneo hilo.

‎Sambamba na hilo, Mkurugenzi wa Shirika ka Helen Keller International Dkt. Geogle kabona amesema msaada huo utaendelea kutolewa pamoja na kutoa huduma ya mafunzo kwa wataalamu wa eneo hilo pamoja na kutolewa kwa elimu ili jamii ipate uelewa huo.

‎"Tutaendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kupunguza upofu unaozuilika na kuhakikisha wananchi wengiz zaidi wanaoata huduma bira za afya ya macho," amesema Dkt. Kabona

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn