TANZANIA NA MSUMBIJI KUIMARISHA USHIRIKIANO
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Msumbiji (FADM) yamefanya Kongamano la Nne la Ujirani Mwema katika Mkoa wa Mtwara, kuanzia Oktoba 26 hadi 27, 2026, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kudumisha amani kati ya nchi hizo mbili.
Kongamano hilo limeongozwa na Kamanda wa Brigedi ya Kusini (401 KV) wa JWTZ, Brigedia Jenerali Sijaona Myala, pamoja na Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Msumbiji (FADM), Rear Admiral BE Nchokomala.
Katika kongamano hilo, pande hizo mbili zimejadili masuala mbalimbali, yakiwemo mikakati ya kuimarisha ulinzi wa mpaka wa Tanzania na Msumbiji pamoja na kuendeleza uhusiano mwema na ushirikiano kati ya majeshi hayo.
.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa mikutano iliyotangulia yenye lengo la kuimarisha ujirani mwema, amani na usalama wa nchi hizo mbili.
.
Uhusiano wa Tanzania na Msumbiji ulijengwa kwa misingi ya mshikamano, uhuru, amani na ushirikiano wa Afrika chini ya viongozi waasisi wa mataifa hayo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Samora Moisés Machel wa Msumbiji.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

