Top news
TUENDELEE KUULINDA NA KUUTUNZA MUUNGANO WETU -WAZIRI MKUU MAJALIWA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watanzania wote bara na visiwani kuendelea kuulinda,kuuenzi, kujivunia na kuuthamini muungano wetu kwani ni tunu adimu na adhimu inayopaswa kulindwa kwa gharama yoyote.
.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo April 08,2024 alipokuwa akizindua Nembo na KauliMbiu ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
.
Amesema watanzania wana kila sababu ya kujivunia muungano huo kwa kutimiza umri wa miaka 60 na ni ukweli usiopingika kwamba muungano wetu umeendelea kuwa na tija kubwa na kuchagiza maendeleo ya nchi yetu na wananchi wote kwa ujumla.
.
"Muungano wetu umefanya Tanzania liwe Taifa lenye utulivu, mshikamano, nguvu na mfano kwa mataifa mengi barani Afrika na duniani kwa ujumla" alisema Majaliwa.
.
Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wananchi wote kutumia maadhimisho hayo kutafakari tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi tangu muungano uliopoasisiwa mwaka 1964.
.
Aidha,Majaliwa Amewasihi wananchi wote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwachagua viongozi wanaotosha,ili wasaidie kuharakisha maendeleo yetu hapa nchini.
.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Joakim Mhagama (Mb) amesema katika Miaka 60 ya Muungano,miradi ya maendeleo itazinduliwa na viongozi wakuu wa kitaifa pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mawaziri na Wakuu wa Mikoa hivyo, amewaomba mawaziri wote nchini kushiriki ipasavyo katika uzinduzi wa Miradi hiyo watakayopangiwa kuzindua ikiwa ni pamoja na kuambatana na viongozi wa Kitaifa katika uzinduzi wa miradi watakayoizindua.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma amesema Muungano huo kudumu kwa miaka 60 sio jambo jepesi, tayari kuna misukosuko mingi ambayo muungano huo umepitia, mathalani kwenye Bunge la Katiba, kuna watu waliukana muungano kuwa haupo kwa sababu hakuna hati ya muungano.
.
Aidha,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Seleman Said Jafo (Mb) amesema katika Miaka 60 ya Muungano, tuna sababu ya kuwashukuru viongozi wetu wakuu kwa kutuheshimisha sana,kwa sababu katika kipindi chao cha miaka mitatu wameweza kutatua kero 15 za muungano kati ya kero 18 zilizokuwa zimebakia.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

