logo

RAIS DKT.MWINYI AAHIDI FIDIA ZITALIPWA KWA KILA MWANANCHI WA MANGAPWANI NA BUMBWINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itakikisha kila mwananchi atapewa nyumba nzuri kuliko anayoishi sasa ikiwa ni fidia kwa nyumba zao.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa nyumba ikiwa ni fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa barabara na bandari ya Mangapwani Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini tarehe 24 Novemba 2023.

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kila mwananchi anayestahili kulipwa fidia ikiwemo ya mazao na majengo Serikali itahakikisha fidia hizo zinalipwa kulipwa kwa Mangapwani wameshalipwa na Bumbwini uthamini unaendelea na watalipwa siku chache zijazo.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema kila mwananchi atapata haki yake hataki kusikia watu wanadhulumiwa haki zao.

@ikulu_habari

#JordanMediau

pdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn