TBA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA MABANDA YAO KWENYE MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI MKOANI GEITA
Wakala wa Majengo
Tanzania(TBA)imeshiriki Maonesho ya Sita (6) ya kimataifa ya teknolojia ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita kwa Mwaka huu yaliyoanza tangu Septemba 23,2023 Katika viwanja vya EPZ BombaMbili.
.
TBA imeshiriki kwa ajili ya kuonesha Shughuli mbalimbali zinafanywa na wakala huo kama vile, katika idara ya Ushauri wanatoa huduma za Ubunifu, Ushauri pamoja na usimamizi wa miradi yote ya ujenzi ya majengo ya Serikali.
.
Na pia katika idara ya milki, Wakala wa Majengo Tanzania unasimamia pamoja na kuendeleza milki za Serikali.
.
Aidha, kwa upande wa Idara ya Ujenzi, TBA inasimamia shughuli za Ujenzi na kujenga majengo ya Serikali,nyumba za watumishi,nyumba za viongozi pamoja na kudhibitisha ubora wa Majengo hayo.
.
TBA inawakaribisha wananchi wote kujitokeza katika mabanda yao ili kujionea mambo mbalimbali wanayoyafanya kupitia ujenzi.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

