logo

SERIKALI KUPITIA TANESCO INAFANYA JITIHADA ZOTE KUHAKIKISHA UMEME UNAPATIKANA NCHINI - MHE.KAPINGA

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inafanya jitihada zote katika kuhakikisha Watanzania wote wanapata umeme wa uhakika.

Mhe.Kapinga amesema hayo, Septemba 11, 2023 wakati akizungumza baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukamilisha ziara yake kwenye vyanzo vya kuzalisha umeme vya Kihansi, Mtera na Kidatu.

"Tulianza Mtera, tukaja Kihansi na sasa Kidatu lengo ni kuangalia namna umeme unavyozalishwa, namshukuru Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson kuruhusu kamati hii ije Kukagua maeneo haya muhimu katika uzalishaji umeme nchini," amesema Mhe. Kapinga.

Aidha, amesema hali ya uzalishaji umeme imetengemea na Serikali kupitia Tanesco inafanya jitihada zote kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika.

Kuhusu utunzaji wa mazingira, Mhe. Kapinga amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi Bilioni 5 ajili ya utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo vya Maji.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Ussi Salum Pondeza amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Tanesco na kusisitiza suala la utunzaji wa mazingira ili kutunza vyanzo vya maji kuepuka upungufu wa huduma ya umeme.

.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn