TIC YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUBORESHA UWEKEZAJI NCHINI
KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza ma waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya Madini Ruangwa mkoani Lindi ,Afisa Mwandamizi Muhamasishaji wa uwekezaji wa ndani Latifa Kigoda amesema moja ya maboresho aliyoyafanya ni pamoja na kuweka misamaha ya Kodi kwa wawekezaji Ili wageni na wazawa waweze kufanya uwekezaji hapa nchini.
"Tupo kwenye maonyesho haya kuwaletea habari njema kutoka kwa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kwamba ameboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kupunguza mahitaji ya yakuweza kujisajili na TIC."amesema na kuongeza kuwa,
"Hapo awali ilikuwa ili mwekezaji akidhi mtaji wakuweza na kujisajili TIC, lazima thamani ya mradi wake iwe milioni 200 ila baada yakuonekana muamko wa wazawa kuwa mdogo Mheshimiwa Rais amepunguza kutoka milioni 200 Hadi kufikia shilingi milioni 100.
"Pia ninaomba niwafahamishe wana Lindi kituo cha Uwekezaji Tanzania siyo Taasisi ya wageni peke yao kama wengi wanavyodhani,bali TIC ni kwa ajili ya wazawa pia."amesema Latifa.
Kwa upande wake Afisa Mwekezaji Mkuu TIC Kanda ya Mashariki Griyson Mtimba amewashauri wawekezaji nchini kusajili miradi yao kupitia kituo cha uwekezaji TIC ili waweze kupata msamaha wa kodi inayotolewa na Serikali kupitia TIC.
Amesema TIC wapo katika maonyesho ya madini na uwekezaji yanayofanyika katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kwa ajili kutoa Elimu na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje wawese kuwekeza hapa nchini.
"TIC tuna jukumu la kufanikisha uwekezaji kwa kutoa vibali mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo NIDA,Uhamiaji, OSHA na Taasisi nyingine .
Aidha,Mtimba amesema kuwa kupitia maonyesho hao muitiko umekuwa mkubwa hasa kwa wawekezaji wa ndani ambapo wamewapa elimu ya uwekezaji na namna nawaweza kusajiri miradi TIC.
"Tunawahamasisha wawekezaji wa ndani waje wasajili miradi yao TIC, huku kuna punguzo la kodi hasa wanapoaagiza vifaa vyao kutoka nje ya nchi nasi kama TIC tupo tayari kushirikiana nao, hasa wakishapata cheti cha uwekezaji kutoka TIC ikiwemo vifaa vyakuchakata madini na miradi mbalimbali"amesema Mtimba
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

