logo

MHANDISI ARON: UCHIMBAJI VISIMA ENEO LA NZUGUNI UMEKAMILIKA ASILIMIA 100%

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi.Aron Joseph Amesema Uchimbaji Wa Visima vya Maji Katika Eneo la Nzuguni Umekamilika Kwa Asilimia 100%, na Visima vimeshachimbwa vitano (5) na Maji wameyapata Lita Milioni 7.6 ambayo wanaweza kuyazalisha Kwa Siku na yatakwenda kuwapunguzia uhaba Wa Maji Kwa Asilimia 11.7.

.

Aron Ameyasema Hayo Alipokuwa akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 28, 2023 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

.

Aron Amesema Kuhusu Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wanakwenda Kuhakikisha Chuo hicho kinapata Maji Ya Kutosha Ili kusiwepo na Migao Katika Eneo Hilo.

.

"Tunataka Kuongeza Maji Katika Eneo la Chuo Kikuu Cha Dodoma, Chuo hiki kina Uwezo Wa Kuchukua Watu wasiopungua Elfu 45,000 na Kwa Hivi Sasa hakijafikia Uwezo Wa Kuchukua Watu Wote kwahiyo Wapo Watu Elfu 35,000 Na Maji tunayoyapeleka ni wastani Wa Lita 70 Kwa Kila Mtu Kwa Siku. kwahiyo tunatakiwa tuongeze mpaka Lita 120 hapo Ndipo Chuo kitakuwa Salama" Amesema Aron.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema watachimba Visima vya Maji Eneo la Nala,Michese na Veyula Kwa Ajili ya Kuongeza Maji yanayokuja Katikati ya Jiji, Kwahiyo Huo Ndio Mpango Wa Dharura unaokwenda Kupunguza Tatizo la Maji.

.

Amesema Miradi Yote hiyo inakwenda Kuhakikisha Kwamba wanaongeza Huduma Ya Maji Kufikia Asilimia 93% Ndani ya Mwaka 2024, na Pia wanakwenda Kuongeza muda Wa Huduma Kutoka Masaa 13 mpaka 19.

.

Aidha, Aron Amesema Kupitia Mradi Wa Miji 28 Tanzania Bara Na Visiwani imetengewa Bilioni 17, na Fedha Hizo zinakwenda Kuongeza Matenki ya Maji, Visima vya Ziada na Pia zinakwenda Kuhakikisha Maeneo Yote ya Chamwino yanapata Maji.

.

"Kupitia Fedha Hiyo, Chamwino inakwenda Kupata Maji Kwa Masaa 24 Kwa Asilimia 100% Na inakuwa Salama Kwa miaka 30 ijayo" Amesema.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn