logo

DC HALIMA AGAWA VISHIKWAMBI WATENDAJI WA KATA 26 BAGAMOYO

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Halima Okash(@okash_halima) Ametoa Vishikwambi (Tablets) Kwa Watendaji wa Kata zote 26 za Wilaya hiyo ili waweze kutatua changamoto ya Mawasiliano na kuongeza ufanisi wa kiutendaji.

.

Okash pia Ametoa vishkwambi hivyo kwa Maafisa Tarafa waliofanya vizuri kwenye maeneo yao, Kwa sababu hiyo ameamua kuwapatia vishkwambi (Tablets).

.

Utoaji Wa Vishikwambi hivyo Umekuja mara Baada ya kuzunguka kwenye kata zote 26 za Wilaya hiyo (Halmashauri ya Chalinze na Halmashauri ya Bagamoyo), na kugundua changamoto ya mawasiliano kama moja ya kikwazo kinachopunguza ufanisi wa utendaji.

.

Aidha, Mkuu Huyo Amesema Ni imani yake kuwa vitendea kazi hivyo alivyogawa siku ya Jana Julai 25,2023 itakua chachu ya kurahisisha mawasiliano, lakini pia motisha kwa watendaji wenzake wote ili waweze kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo kwa ufanisi na kasi zaidi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn