Top news
WANAWAKE SIMAMIENI MAADILI YA JAMII YETU- RAIS SAMIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassan Amewataka Wanawake kushikamana na Kuilea Jamii Katika malezi yaliyo Bora kimaadili Ili kujiepusha Jamii Na Vitendo Viovu.
.
Rais Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 16,2023 Katika Kongamano la Wanawake wa Kiislam Zanzibar Mwezi 27 Katika Maadhimisho Ya Mwaka Mpya Wa Kiislamu 1445- Hijjiria lililofanyika Katika Ukumbi Wa Golden Tulip.
.
Amesema Kila Mwanamke ana Wajibu wa Kusimamia Maadili Kwa Kuwa ana Mchango mkubwa Sana Katika Kujenga au Kumomonyoa Maadili Ya Familia na Jamii Kwa Ujumla.
.
Kwa Upande Mwingine, Rais Samia Amesema hivi Sasa Wanawake wamekuwa Mstari Wa Mbele Kupigania Haki na Kushiriki Katika Masuala Ya Kitaifa na Kijamii Kwa Kufanya Kazi Kwa Uadilifu, uhakika Na weledi mkubwa ambazo Awali walidhaniwa hawawezi.
.
Aidha, Rais Samia Amewataka Wanawake kuiepusha na Vitendo Vya unyanyasaji Kwa Kuwa Vinarejesha Nyuma Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa Na Kijamii.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

