logo

RAIS DKT.KIKWETE: JKT ENDELEENI KUBUNI NA KUANZISHA MASHINDANO MBALIMBALI

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ametoa Rai Kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kuendeleza Jitihada za Kubuni Na Kuanzisha Mashindano Ya Riadha na Michezo Mingine Ili Kuendeleza na Kukuza Vipaji Vingi Zaidi.

.

Kikwete Ameyasema Hayo Leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akizungumza Wakati Wa Mbio za JKT (JKT Marathon)Tukio lililofanyika Katika Uwanja Wa Jamhuri Dodoma, Kuelekea Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo Maadhimisho Yake Yanatarajia kufanyika Mwezi Julai 2023.

.

Amesema Madhumuni ya Mbio Hizo (JKT Marathon) ni Kuitangazia Nchi Na Dunia Kwamba Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linatimiza Miaka 60 Tarehe 10 Julai 1963 Jeshi Hilo lilianzishwa na Tangu Kuasisiwa Kwake, JKT imefanya mambo mengi mazuri na Yenye Maslahi Mema Kwa Nchi Yetu.

.

"Tumeshuhudia Mafanikio Katika Malezi Ya Vijana, Pamoja Na Ulinzi na Usalama. JKT ni Chombo Cha Uzalishaji Mali, wanalima,Wana Viwanda, wanafuga na wanasaidia Katika kukuza Uchumi Wa Nchi" Amesema Dkt. Kikwete.

.

Dkt.Kikwete Amesema Kwa Upande wa Michezo, JKT wamekuwa wakiitoa Nchi Yetu kimasomaso ambapo Wana Michezo Kutoka Jeshi hilo wamekuwa wakishiriki kwenye Michezo Mbalimbali Ndani na Nje ya Nchi Hususani kwenye Riadha Nchi Yetu imeendelea Kutangazwa Kupitia Kwa Wana Michezo wao.

.

Rais Mstaafu Huyo Amelitaka Jeshi Hilo kuwekeza Kwa Timu Ya Wanawake Ya JKT Queens Ili waweze Kupata Kocha Mzuri, Pamoja Na Wachezaji wazuri Wa Timu hiyo ili iendelee Kufanya Vizuri Zaidi.

.

Aidha, Dkt.Kikwete Amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kwa Kuandaa Mashindano Hayo Na Ana Imani Mbizo Hizo zilizofanyika Leo zitaendelea Kufanyika Kila Mwaka Ili watu wakipata Fursa ya Kufanya Mazoezi itakuwa ni Jambo Jema Sana.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn