Top news
MSIGWA: RIPOTI YA CAG, HAKUNA MTU ATAKAYEACHWA
MSEMAJI Mkuu Wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa, Amesema Mara Baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutolewa, Hakuna kitu kitakachoachwa Pale ambapo kuna taasisi imehusika katika upotevu wa mali za umma hatua kali zitachukuliwa.
.
"Vyombo Vyetu vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanyia kazi maelekezo ya Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kufanya uchunguzi kwenye maeneo yote ambayo CAG ameyatolea taarifa"
.
Msigwa Ameyasema hayo April 19,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akitoa Taarifa Ya Utekelezaji Wa Shughuli za Serikali Kwa Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma.
.
Amesema Ripoti ya CAG ni moja ya nyenzo ambazo Serikali inazitumia katika kusimamia rasilimali za Watanzania, pia inatumika katika kuangalia ni maeneo gani yanahitaji kuongezewa nguvu katika usimamizi wa rasilimali za Watanzania na hatua gani zinapaswa kuchukuliwa ili rasilimali hizo ziendelee kuwa salama.
.
Msemaji Huyo Amesema Daraja la Kigongo - Busisi kazi inaendelea, mradi upo zaidi ya 70%, ujenzi wa barabara ya mzunguko iliyopo jijini Dodoma umefikia 18% na ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere umefikia 85.6%. Mwezi Juni, 2024 tunaweza kuanza kuzalisha umeme.
.
Aidha, Msigwa Amesema Kamati ya Uchumi ya kuchunguza uchumi wa vyombo vya habari inaendelea na kazi, muda wowote tarehe ya kukutana na wadau wa makundi yote ya wadau wa vyombo vya habari wakiwemo Wamiliki, Vyama vya Waandishi wa Habari, wanamitandao n.k itatangazwa.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

