logo

NDUMBARO: WEKENI JUHUDI KATIKA MAJUKUMU YENU

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro amewahasa watumishi wa Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka juhudi katika kutekeleza majukumu yao ili kulinda taswira ya jamii na kuwa chachu ya mabadiliko.

.

Ndumbaro Ameyasema Hayo alipokuwa Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Takwimu Jijini Dodoma Tarehe 18 Aprili,2023.

Katika Mkutano huo wenye lengo la kuwapitisha watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Taarifa ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 ya Ofisi hiyo ambapo watumishi watapata wasaa wa kuchambua vipambele vya mpango na bajeti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mwaka 2023/24 ili kuhakisha mafanikio yaliyofikiwa mwaka 2022/2023 yanaongezeka.

Vile vile Ndumbaro ametoa rai kwa viongozi wa Baraza hilo kutumia Baraza hilo kama njia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

@maelezonews

@katibanasheria_

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn