POLISI KATA AJITOLEA KUMHUDUMIA MAMA MWENYE ULEMAVU NA MWANAE
Polisi Kata wa Lubanga, INSP Paschazia Nunda, amejitolea kufuatilia kwa karibu afya na ustawi wa mama mwenye ulemavu, Elizabeth Nghungu, pamoja na mtoto wake wa kiume aliyejifungua hivi karibuni.
.
Katika ziara hiyo iliyofanyika akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mwabagalu, INSP Paschazia alimtembelea Elizabeth nyumbani kwake kwa lengo la kumjulia hali na kumpa faraja.
.
Amesema ataendelea kuhakikisha mama huyo na mtoto wake wanapata huduma muhimu za afya, ikiwemo kufuatilia mahudhurio ya kliniki kwa wakati, ili kulinda afya na maendeleo yao.
.
Kwa upande wake, Elizabeth ameishukuru na kuipongeza Jeshi la Polisi kwa upendo na msaada alioupata, akisema hatua hiyo imempa faraja na kuonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya polisi na jamii.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

