logo

DEREVA AKAMATWA BAADA YA BASI KUTUMBUKIA MTONI MIKUMI,ABIRIA 13 WAJERUHIWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva Charles Hirali Msangi (34), mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali iliyosababisha majeruhi kwa abiria kadhaa.

‎.

‎Ajali hiyo iliyotokea usiku wa Aprili 16, 2026 katika eneo la Daraja Namba Saba, Ruaha, Tarafa ya Mikumi, Wilaya ya Kipolisi Ruhemba, mkoani Morogoro, kwenye barabara kuu ya MikumiKilombero.

‎.

‎Inadaiwa kuwa basi lenye namba za usajili T 289 EAG, aina ya San Long, mali ya Kampuni ya Laviha, lililokuwa likifanya safari kutoka Ifakara kuelekea Dar es Salaam likiwa na abiria 57, lilitoka nje ya njia, kutumbukia mtoni na kupinduka.

‎.

‎Kutokana na ajali hiyo, abiria 13 walijeruhiwa, wakiwemo wanaume 10 na wanawake watatu. Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya kwa matibabu na baadaye kuruhusiwa kurejea majumbani kwao.

‎.

‎Aidha, Jeshi la Polisi Morogoro limetoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn