logo

MWANARIADHA GOUT GOUT AVUNJA REKODI YA DUNIA KWA KUKIMBIA MITA 200 KWA SEKUNDE 19.67 AUSTRALIA

Mwanariadha chipukizi wa Australia, Gout Gout mwenye umri wa miaka 18, ameandika historia mpya baada ya kukimbia mita 200 kwa muda wa sekunde 19.67 katika mashindano ya taifa yaliyofanyika Sydney.

‎.

‎Muda huo umevunja rekodi ya dunia kwa vijana (junior) na kumweka kileleni mwa orodha ya wanariadha chipukizi wenye kasi zaidi duniani kwa sasa.

‎.

‎Kinachovutia zaidi ni kwamba muda huo ni wa haraka kuliko ule ambao gwiji wa mbio fupi Usain Bolt aliukimbia akiwa na umri kama huo, ambapo mwaka 2005 alishuka chini ya sekunde 20 kwa mara ya kwanza kwa kukimbia 19.99.

‎.

‎Matokeo haya yanatuma ujumbe mzito katika ulimwengu wa riadha kwamba kizazi kipya cha kasi kimeanza kuonekana, na ubora hauhitaji kusubiri muda mrefu kujidhihirisha.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn