logo

EBENEZA AFUNGWA JELA MWEZI MMOJA ‎KISA WIZI WA GARI LA POLISI GHANA

Mwanaume mwenye umri wa miaka 26,raia wa nchini Ghana, Ebenezer Frimpong, amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela baada ya kukiri kosa la kujaribu kuiba gari la Polisi katika Mkoa wa Ashanti nchini humo.

‎.

‎Mahakama ya Kwadaso Circuit Court iliyopo Kumasi ilitoa hukumu hiyo baada ya Frimpong kubadili kauli yake na kukiri kosa, huku ripoti ya madaktari wa afya ya akili ikibaini kuwa alikuwa na uwezo wa kusimama kizimbani.

‎Kwa mujibu wa taarifa za mahakamani, tukio hilo lilitokea Mwezi Aprili 14, 2026, wakati askari aliyekuwa akisafirisha gari hilo kwenda karakana alisimama karibu na Soko la Nkawie kununua dawa, na kuliacha gari bila ulinzi.

‎Inadaiwa Frimpong alichukua fursa hiyo na kuondoka na gari hilo, lakini polisi walimkamata muda mfupi baadaye karibu na eneo la Mim na kulirejesha gari hilo bila kuharibika.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn