logo

TANROADS YAANDIKA HISTORIA KWA KUHAMISHIA RASMI WATUMISHI MAKAO MAKUU DODOMA

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeandika ukurasa mpya katika historia yake kwa kufanya hafla maalumu ya kuwakaribisha Watumishi waliohamia rasmi katika Makao Makuu ya Serikali, Dodoma.

‎.

‎Akizungumza katika hafla hiyo leo Agost . 01.2026 Mtendaji Mkuu Mha.Mohamed Besta aliwakaribisha kwa moyo mkunjufu watumishi wote waliohamia Dodoma na kueleza kuwa Uongozi unatambua kuwa mabadiliko ya makazi na mazingira ya kazi si jambo rahisi.

‎.

‎Aliwahimiza watumishi kuwa na Moyo wa uvumilivu na mshikamano wanapoanza maisha mapya katika jiji hilo, akisisitiza kuwa uongozi utaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao.

‎.

‎Aidha, Mtendaji Mkuu alitangaza kuwa kuanzia sasa TANROADS itaendelea kutekeleza rasmi majukumu yake kutoka Makao Makuu yaliyopo Dodoma, hatua inayoendana na utekelezaji wa sera ya Serikali ya kuhamishia shughuli zake katika mji mkuu wa Nchi.

‎.

‎Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi wa Dini waliotoa Dua na Sala za kuwatia moyo watumishi waliohamia Dododma,pamoja na mameneja wa Idara.

‎.

‎Pia watumishi kutoka TANROADS Mkoa wa Dodoma walikuja kuwakaribisha watumishi wenzao katika hafla hiyo kwa kushiriki chakula cha pamoja kilicho andaliwa na Mtendaji Mkuu.

‎.

‎Hafla hiyo ilifuatiwa na upandaji mti wa kihistoria wa uzinduzi wa Ofisi Njedengwa uliopandwa na Mtendaji Mkuu.

‎.

‎Katika kuonesha umuhimu wa ustawi wa watumishi, mtaalamu wa afya ya akili Daktari Nuruel Kitomari pia alialikwa kutoa mada iliyolenga kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mabadiliko, msongo wa mawazo na namna ya kuimarisha afya ya akili wakati wa kuzoea mazingira mapya ya kazi na maisha.

‎.

‎Hafla hiyo imebeba ujumbe wa umoja, matumaini na mwanzo mpya, huku ikiashiria hatua muhimu katika safari ya TANROADS ya kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kutoka Makao Makuu yake mapya jijini Dodoma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn