logo

TANZANIA NA KOREA KUENDELEZA USHIRIKIANO SEKTA YA MIUNDOMBINU

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amekutana na kufanya mzungumzo na Makamu wa Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Hyun Hwan Jin pamoja na ujumbe wake leo, tarehe 27 Mei, 2025 katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Serikali ya Tanzania imeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwakuendeleza ushirikiano katika maeneo mbambali ikiwemo ufadhili wa ujenzi wa Daraja la Tanzanite, jijini Dar es Salaam lenye urefu wa kilometa 1.03 na Barabara unganishi Kilometa 5.2 ambalo limekamilika na linatumika.

Aidha, Naibu Waziri Kasekenya amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Taasisi za Korea za K-FINCO pamoja na KIND na Taasisi za TBA na TANROADS zilizo chini ya Wizara hiyo ambao unajikita kwenye ufadhili wa miradi ya ujenzi wa miundombinu na miradi ya ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP).

Kwa upande wake, Makamu wa Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Jamhuri yaKorea, Mhe. Hyun Hwan Jin ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wanaowapa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo na kuona namna makampuni ya Ujenzi ya Korea Kusini yanavyoweza kushiriki katika miradi ya ujenzi wamiundombinu ya Barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari na uendelezaji wa miji na majiji nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara na Taasisizake ikiwemo TBA, TANROADS na TEMESA.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn