MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA KUTUA BUNGENI
SERIKALI inatarajia kupeleka Bungeni MUSWADA wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa hivi karibuni ili kuamua umri sahihi wa watoto wa kike kuingia kwenye ndoa.
Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ali Khamis akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Dkt. Thea Antara bungeni leo tarehe 18 Aprili, 2023 aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuamua juu ya wasichana kuolewa chini ya Mika 18.
"Sheria ya mtoto namba 21 ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 inamtambua mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni mtoto. Hivyo ni kosa la jinai kumuhusisha na mahusiano ya kimapenzi pia kumuozesha, Kwa upande mwingine sheria ya ndoa ya Mwaka 1971 inaruhusu mtoto wa kike kuingia wenye ndoa akiwa na miaka 14" amesema Mhe. Mwanaidi.
Naibu Waziri Mwanaidi ameongeza kwamba Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeshakusanya maoni kutoka kwa Wadau kuhusu upi umri sahihi wa kuoa au kuolewa.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akijibu swali la nyongeza amesema tayari maoni ya Wadau yamepokusanywa na kuchambuliwa, hatua inayofuata ni MUSWADA kuwasiliswa Bungeni kwa ajili majadiliano ya kurekebisha sheria hiyo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news