logo

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATOA MAFUNZO KWA KAMATI YA ULINZI MKOANI KATAVI

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Katavi imetakiwa kusikiliza vizuri na kwa weledi mafunzo yanayotolewa na Wizara ya katiba na sheria na kuhakikisha wanayatumia kwa kutatua kero,matatizo,migogoro na mambo mbalimbali yanayohusu wananchi kwenye maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwamvua Mrindoko wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika mpanda katika ukumbi wa mkuu wa mkoa huo.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa sababu yatamuongezea kila mmoja uelewa zaidi wa namna gani ya kusimamia wananchi,kuongoza na kusimamia watumishi na viongozi ndani ya vyombo hivyo vya dola katika kuimarisha uzingatiaji misingi ya utawala bora,haki za binadamu Pamoja na usalama ndani ya mkoa huo.

"Elimu tutakayopata hapa leo ninaamini kabisa itasaidia kwenda kutoa elimu zaidi kwa wananchi pamoja na kwamba kila chombo hapa kinaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mambo ya uvunjifu wa maadili masuala ya kujichukilia sheria mkononi,mauaji pamoja na mila potofu"

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn