BARABARA YA PAWAGA MPAKA IZAZI KUJENGWA KWA LAMI HATUA KWA HATUA -WAZIRI LUKUVI
Imeelezwa kwamba barabara ya Pawaga mpaka Izazi imewekwa katika mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami hatua kwa hatua ili kurahisisha shughuli za mawasiliano na kuchochea shughuli za uchumi kwa wananchi wa Isimani.
.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani wakati alipofanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya Makuka, Izazi na Mnadani vilivyopo katika kata ya Izazi Jimbo la Isimani Mkoani Iringa leo tarehe 25 Mwezi Novemba 2024.
.
Amefafanua kwamba ingawa barabara hiyo inachongwa kwa sasa lakini Serikali ya Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kutoa fedha kwa awamu na kuanza ujenzi wa lami katika upande wa Pawaga kuelekea Izazi.
.
Alisema “barabara hiyo yenye urefu wa KM 25 ni barabara muhimu kwa wananchi na hasa katika usafirishaji wa mazao lakini pia itasaidia wananchi kufika kwa urahisi katika hospitali ya wilaya kujipatia huduma za afya.
.
"Naomba niwatoe wasiwasi wananchi utejekelezaji wa miradi ya maendeleo inaenda kwa hatua na serikali imejipambanua katika kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea kama ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoeleza" alisema.
.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Izazi Mhe. Constatino Makala ameishukuru Serikali kwa kuweka taa za barabarani katika kijiji cha Izazi jambo linalosaidia wananchi kupata fursa na mazingiza mazuri ya kujishughulisha na biashara.
.
“tumekusudia kuendelea kuwahamasisha vijana wanaojishughulisha na shughuli za nyamachoma na mamalishe katika baraba ya Iringa Dodoma ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa kwa makundi ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu isaidie katika kuboresha shughuli zao za biashara.” alisema.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news