MABULA: WANA TARIME ACHENI KUISHI KWA MAZOEA, FUATENI SHERIA
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Kegonga na Karakatonga wilayani Tarime mkoa wa Mara kuacha kuishi kwa mazoea na kufuata sheria ili kuepuka migogoro baina ya vijiji hivyo na maeneo ya hifadhi.
Mabula amesema hayo tarehe 6 Mei 2023 katika kijiji cha Kegonga kitongoji cha Lisolya kata ya Nyanungu wilayani Tarime, wakati timu ya mawaziri watatu ilipotembelea eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa kuwataka mawaziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kwenye wilaya za Tarime na Serengeti mkoani Mara.
Mawaziri waliotembelea vijiji hivyo ni Angellah Kairuki, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mary Masanja.
Vijiji vilivyopo kwenye mgogoro na eneo la Hifadhi ya Serengeti wilayani Tarime mkoa wa Mara ni Kegonga, Nyandage, Masanga, Karakatonga, Gobaso, Nyabirongo pamoja na Kenyamosabi.
Waziri Huyo amewaambia wananchi wa vijiji hivyo kuwa, kitendo cha timu ya mawaziti watatu kwenda eneo la mpaka lenye mgogoro ni ishara kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amewaheshimu wananchi wa maeneo hayo.
Mabula Amewataka wananchi wa mkoa wa Mara kuacha ubishi na kufuata sheria huku akiwatahadharisha dhidi ya watu wanaokwenda kuwadanganya na kueleza watu hao wana lengo la kutafuta kura wakati wa uchaguzi na kueleza kuwa iwapo wataishi kwa kukubali kudanganywa waelewe kuwa mpaka baina ya vijiji hivyo na hifadhi utaendelea kubaki kama ulivyo.
Aidha, Mabula Amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kuheshimu kile ambacho kipo kwa mujibu wa sheria na kueleza kuwa GN 265 ya mwaka 1968 ambayo wao wanaitambua ndiyo iliyotafsiriwa na si vinginevyo na kuhoji wanachoshangaa ni kitu gani.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

