logo

WAHITIMU FORM SIX AMBAO BADO HAWAJARIPOTI MAKAMBINI WAKARIPOTI MARA MOJA -BRIGEDIA JENERALI MABENA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawataka vijana wote walioitwa awamu ya kwanza ambao hawajaripoti makambini mpaka sasa, waripoti mara moja katika makambi yaliyo karibu na makazi yao.

.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Juni 22,2024 katika ukumbi wa Mabeyo Complex kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesema JKT imetoa nyongeza ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita 2024 kujiunga na JKT ili kufanya mafunzo hayo ya lazima.

.

Brigedia Jenerali Mabena amesema vijana hao wote wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia leo hii tarehe 22 Juni 2024 hadi tarehe 26 Juni 2024.

.

Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo awamu ya pili na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

.

Aidha,Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, anawakaribisha vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024 kuungana na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo,Umoja wa kitaifa, Kufundishwa stadi za Kazi,Stadi za Maisha na Utayari wa Kulijenga na Kulitumikia taifa lao.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn