logo

MEJA JENERALI MABELE AHITIMISHA ZOEZI LA UFUNGAJI MAFUNZO YA AWALI YA VIJANA WA JKT RWAMKOMA MKOANI MARA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele amehitimisha zoezi la ufungaji wa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni Miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Rwamkoma JKT kilichopo Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Akitoa hotuba yake, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.

"Serikali imekuwa ikiboresha miundo mbinu ya Makambi na Vikosi vya JKT ili kuliwezesha Jeshi hili kuchukua vijana wengi zaidi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo". Aliongeza Meja Jenerali Mabele.

Aidha, Meja Jenerali Mabele alipata wasaa wa kuzindua rasmi mitandao ya kijamii ya JKT ambayo ni X, Instagram na Facebook ili kuupa wigo Umma wa watanzania kupata habari mbalimbali zinazohusu JKT.

"Kwakuwa dunia kwa Sasa ipo kiganjani hivyo nasi JKT tunalitambulisha jukwaa la mitandao yetu ya kijamii kuwa moja ya eneo ambalo jamii itaweza kupata habari zetu kwa uhakika, mbali na ile njia ya Tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz inayoendelea kutumika."

Akitoa salamu za Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkurugenzi wa Utumishi kutoka Tawi la Utumishi Jeshini Brigedia Jenerali Simon Pigapiga amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri na kujiepusha na vitendo viovu.

"Niwasihi mkawe vijana bora wakati wote kwa kujiepusha na vitendo viovu vitakavyo wasababishia matatizo ya afya ya mwili na akili". Alisema Brigedia Jenerali Pigapiga.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar, Kanali Makame Daima amesema kuwa JKU inaendelea kujifunza kutoka kwa JKT kutokana na ushirirkiano uliopo baina ya vyombo hivyo viwil.

Naye Kamanda Kikosi Luteni Kanali Gaudencia Mapunda amesema mafunzo waliyoyapata vijana hao yamewajengea Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji kwa Taifa lao.

Akisoma risala mbele ya mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya wahitimu wenzake, Service Girl Irimina Adolph amesema mafunzo ya JKT waliyoyapata wamefanikiwa kujengewa uzalendo, Nidhamu, Ukakamavu na Umoja wa Kitaifa.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn