UWANJA WA NDEGE WA MSALATO DODOMA UKAMILIKE KWA WAKATI HUSIKA -PROF.MAKAME MBARAWA
Waziri wa Uchukuzi Mhe.Prof.Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma mpaka hivi sasa umefikia asilimia 47 kwa upande wa njia ya kurukia ndege (run way), na kwa upande wa jengo asilimia 12.
.
Prof.Mbarawa ameyasema hayo leo February 7,2024 alipokuwa ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja huo uliopo Msalato jijini Dodoma.
.
Amesema Uwanja huo utakuwa na ukubwa sawa sawa na Uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam au Zanzibar ambapo utakuwa na urefu wa kilometa 3.6.
.
"Uwanja huu utakuwa na sifa ya kipekee, utakuwa na vifaa vya Kisasa vya kuongozea ndege, kutakuwa na taa za instrument Landing System" alisema.
.
Kwa upande wa jengo la abiria, Waziri Mbarawa amesema litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria Milioni 1.5 kwa mwaka, na Control Tower itakuwa na urefu wa mita 56.
.
Aidha, Prof.Mbarawa amewaomba wasimamizi wa mradi huo wa Uwanja wa ndege kuhakikisha wanapambana ili uweze kukamilika kwa wakati.
.
"Tumekubaliana Mradi huu umalizike Mwezi Mei 2025, hasa ule wa jengo. tunaamini tukijipanga na tukisimamia vizuri mradi huu utamalizika kwa wakati, kwa sababu hakuna shida ya fedha" alisema Prof.Mbarawa.
.
Kwa Upande wake Meneja Ofisi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Mhandisi Zuhura Amani amesema wataendelea kumsimamia mkandarasi kuhakikisha kwamba kazi zote muhimu awe amekamilisha kama walivyokubaliana kulingana na mkataba husika.
.
"Tumeyapokea maelekezo yote ya Mhe.Waziri na tunaahidi tutaendelea kumsimamia mkandarasi kwa ukaribu zaidi" alisema Mhandisi Zuhura.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

