logo

WAZIRI BASHUNGWA: JUMLA YA KILOMITA 20 ZA BARABARA ZIMETENGWA KWA AJILI YA MAKANDARASI WANAWAKE

Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024,Jumla ya kilometa 20 za barabara zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wanawake, ambapo zitagawanywa katika vipande vya kilometa tano tano, na kazi hizo zitashindanishwa kwa makampuni ya wanawake peke yao.

"Hii inafanya jumla ya km 220 kujengwa na makandarasi wazawa kwa mwaka 2023/24" amesema.

.

Bashungwa ameyasema hayo leo tarehe 21 Novemba, 2023 katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi wazawa na Washauri elekezi wa ndani Jijini Dodoma, kujadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Center.

.

Amesema Wizara ya Ujenzi, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inaendelea kutenga miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya Makandarasi wa ndani kwa lengo la kuwasaidia Makandarasi hao kukua na kupata uzoefu.

.

“Katika mwaka wa fedha 2023/2024, jumla ya miradi minne ya barabara yenye urefu wa kilometa 50 kila moja zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wa ndani tu, kwa hiyo kilometa 200 zitajengwa na wazawa, hii ni fursa kubwa ya kuwasaidia makadarasi”, amesema Bashungwa.

.

Waziri huyo amesema ameongeza kuwa kazi za matengenezo ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara zenye thamani ya Shilingi Bilioni 600 zitatekelezwa na Makandarasi wa ndani tu katika mikoa yote 26 nchini.

“Katika Mwaka wa fedha 2023/2024 kazi zote za matengenezo ya barabara kwa mikoa yote 26 nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kutekelezwa na Makadarasi wa ndani”, amesema Bashungwa.

.

Aidha,Waziri Bashungwa amefafanua kuwa Sheria ya Ununuzi wa Umma imefanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha thamani ya mradi ambao utatekelezwa na Makandarasi wa ndani tu, bila kushindanishwa na Makandarasi wa nje.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn