logo

KIPANYULA:MAONESHO YAMECHUKUA SURA YA KIMATAIFA

MKURUGENZI Wa Idara Ya Sayansi, Teknolojia Na Ubunifu Kutoka Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula Amesema Katika Wiki Ya Ubunifu iliyoanza Jana April 24 Hadi Kufikia Kilele April 28,2023 wanataka Maonesho Hayo Yachukue Sura ya Kimataifa na Tayari Limeshaanza Kuonekana Hilo.

.

"Mwaka Huu Tumealika waonyeshaji Kutoka Nje Ya Tanzania, Tuna Waonyeshaji Sita (6) Kutoka Africa Kusini Ambao wapo Na Wanaonesha Teknolojia Zao Na Hii Ni Hatua Muhimu"

.

Kipanyula Amesema Hayo Leo April 25,2023 Jijini Dodoma alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kwenye Maonesho Ya Wiki Ya Ubunifu Kitaifa Yanayofanyika Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Hapa.

.

Amesema Kwa Mwaka Huu Katika Maonesho Hayo Kumekuwa Na Ushiriki Wa Makampuni yanayojishughulisha na Masuala ya Sayansi, Teknolojia Na Ubunifu ambapo Wana Makampuni Takribani Sita (6) Yanayoonesha Teknolojia Zao.

.

"Watumiaji Wa Teknolojia Nyingi Ni Viwanda Na Makampuni Mbalimbali kwahiyo Tunafikiri Jukwaa Hili limewezesha Sasa Pande Hizi Mbili Kukutana kuweza Kujadiliana na Kuona Namna Ambavyo Teknolojia Na Bunifu zinazokwenda Sokoni Kwa Kiasi Kikubwa" Amesema Kipanyula.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema Lengo Kuu la Maonesho Hayo Ni Kuonyesha Uwezo tulio Nao kama Nchi Katika Sayansi,Teknolojia Na Ubunifu Na Wanafanya Hivyo Ili kuwawezesha Wabunifu wetu Wa Ndani waweze Kupata Jukwaa la Kukutana Na watumiaji Wa Teknolojia Na Bunifu zinazozalishwa Ndani.

.

Aidha, Kipanyula Amesema Bunifu Nyingi zilizoletwa Katika Maonesho Hayo Ni Zile ambazo zinalenga Kutatua Changamoto zilizopo Katika Jamii.

.

"Tunahamasisha Waendelee kubuni Ili Sasa Tupunguze utegemezi Wa Teknolojia Kutoka Nje Ya Nchi" Amesema Mkurugenzi Huyo.

.

Naye Mkurugenzi Wa Mafunzo Ya Ufundi Stadi Kutoka VETA Ndg. Abdallah Ngadu Ametoa Wito Kwa Wananchi Wote Kujitokeza Katika Maonesho Hayo Ili Kujionea Jinsi Ambavyo VETA inavyotoa Mafunzo Kwa Vitendo, Kwa hivi Sasa Hapa Nchini Wana Vyuo Takribani 50 Ambavyo Vinatoa Mafunzo.

.

"Serikali Imetoa Pesa Kwa Ajili Ya Kujenga Vyuo na Kufikia Mwishoni Mwa Mwaka 2024 tutakuwa Na Vyuo Zaidi Ya 140 Kwa Maana Kila Wilaya Itakuwa Na Chuo. Tunachukua Nafasi Hii Kumshukuru RAIS wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa Kuona Umuhimu Wa Mwananchi Kupata Stadi za Ujuzi Ili aweze Kujiajiri" Amesema Ngadu.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn