logo

DORIS MOLEL: NITATEMBEA KM 5 KWA AJILI YA KUCHANGISHA FEDHA YA UJENZI JENGO LA WATOTO WACHANGA KWIMBA

Siku ya Jumapili ijayo Tarehe 15 Oktoba 2023, Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation Bi.@dorismollel anatarajia kutembea KM 5 kwa ajili ya kuchangisha fedha ya kujenga jengo maalum la watoto wachanga katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

.

Doris anayo furaha kubwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya @jhpiego kwenye kampeni maalum ya #milesformothers mwaka huu kote ambako taasisi hiyo inafanya kazi watatembea kwa ajili ya mradi huo muhimu nchini Tanzania.

.

Aidha, Taasisi ya @dorismollelfoundation inawakaribisha wapenda Afya ya Mama na Mtoto wote kwa shilingi 35,000 tu utajipatia Kit yako na kutembea nao, Mahali : Greenpark Oysterbay Dsm na Bismark Rock Mwanza. 0767803058

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn