logo

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA TUZO YA MALKIA WA MADINI MKOANI GEITA

Serikali imezindua rasmi tuzo ya Malkia wa Madini ya Chama cha Wanawake Wachimbaji wa Madini nchini (TAWOMA) iliyolenga kutambua mchango wa wanawake katika Sekta ya Madini.

Tuzo hizo zimezinduliwa rasmi Septemba 30, 2023 Mkoani Geita na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde zilizokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa TAWOMA

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mhe.Mavunde ameipongeza TAWOMA kwa kuanzisha Tuzo hizo ambazo zitaleta hamasa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa madini.

Aidha, ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kuwa walezi wazuri wa chama hiki na kuwawezesha kufanikisha kuanzishwa kwa tuzo hizi.

Alisema, Serikali kupitia STAMICO imewawezesha wanawake hao kushiriki kikamilifu na kuifanya TAWOMA kuonesha ukomavu ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo TAWOMA ilikuwa ikisuasua.

Aliongeza kuwa, ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na mabilionea wengi wanawake wachimbaji madini nchi nzima kwa kuwa tuzo hizi zinaenda kutia hamasa miongoni mwenu kushiriki kikamilifu kwa kufuata sheria na sera za uchimbaji salama wa madini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella amefurahishwa na jitihada zinazofanyika ndani ya TAWOMA katika kuhakikisha wanawake wengi wanageukia fursa Ilizopo katika Sekta ya Madini.

''Mmemjengea heshima mwanamke mchimbaji na kupitia umoja huu mtazalisha mabilionea wengi na nitaendelea kutoa ushirikiano katika programu hii ya Malkia Wa Madini.

Kwa upande wa STAMICO, ambaye ni mlezi na msimamizi wa wachimbaji wadogo ameipongeza TAWOMA kwa kuwa wabunifu na kuja na Tuzo kama hizi ambazo zinakwenda kuleta matokeo chanya.

Vile vile, TAWOMA ni matajiri wa kesho kwa kuwa kila siku wanaangalia namna ya kuboresha chama ili kiwe na tija kwa wanachama wake nchini.

Kwa upande wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Tanzania (TAWOMA) Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Semeni Malale amesema Tuzo hizi ni matokeo ya harakati za TAWOMA kuhamasisha uchimbaji bora na salama sambamba nakuongea ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn