TUME SPORTS YAIFUNGA TIMU YA MKOA WA MARA
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tume ya Utumishi wa Umma, Tume Sport Club imeibuka na ushindi mnono wa magoli matatu kwa bila dhidi ya timu ya Mkoa wa Mara na kutuma salam kwa washiriki wa mashindano ya SHIMIWI 2023.
Tume imepata ushindi wake wa pili kati ya michezo mitatu iliyocheza katika mashindano ya SHIMIWI mpaka kufikia Oktoba 1, 2023 ambayo yanaendelea kushika kasi Mkoani Iringa
Magoli ya Tume ya Utumishi wa Umma yamefungwa na dakika ya kwanza ya Mchezo na Proches Fabian huku Muhidin Muro akiongeza goli la pili dakika ya 50 kipindi cha pili kisha Proches kurejea tena Nyavuni kuhitimisha karamu hiyo ya Magoli.
Kwa Matokeo hayo Tume Sport Club inarejea katika kilele cha kundi G kwa jumla ya alama 6 na magoli 6 ikifuatiwa na Timu ya Mkoa wa mbeya
Awali Asubuhi kulitanguliwa na mchezo wa kuvuta kamba ambapo timu ya Tume ya Utumishi wa Umma, ilitoka Droo na Timu ya kamba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu
Kwa upande wa Netbal Tume ya Utumishi wa Umma itakua na kibarua kigumu cha kukabiliana na Timu ya Hazina hapo jioni katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

