NAIBU WAZIRI SAGINI: MAGARI RUKSA KUSAFIRI MASAA 24 NCHINI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baada ya kujiridhisha usalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Mhe.Jumanne Sagini (Mb) wakati akizungumza na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.
Ameongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.
Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.
Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

