logo

NDUMBARO: EPUKENI KUIFANYIA SIASA KATIBA,NDIO NGUZO KUU

WAZIRI Wa Katiba Na Sheria Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Amesema Suala la Katiba Mpya Sio Suala Jipya Hapa Nchini hivyo Ametoa Rai Kwa Watu Wote kuepuka Kuifanyia Siasa Katiba na Badala Yake wawe na uvumilivu Kwani Ndio Nguzo ya Nchi Yetu.

.

"Ni kweli Tunahitaji Katiba Mpya Ili Tupate Katiba Mpya, Natoa Rai Kwa Watu Wote kuepuka Kuifanyia Siasa Kwani Katiba Sio Jambo la Kisiasa Wala la Kisheria Bali Ndio Nguzo Ya Nchi"

.

Ndumbaro Amesema Hayo Alipokuwa Kwenye Mjadala Wa 'CLUB HOUSE' Kuhusu Utekelezaji Wa Kampeni Ya Samia Ya Msaada Wa Kisheria Na Jitihada za Kutatua Changamoto za Kisheria Nchini April 22,2023.

Amesema Wizara Yake imeshatoa Mafunzo Kwa Wasaidizi Wa Kisheria Takribani 5000 Nchi Nzima, Na Kati Yao 1000 wameshapata Vyeti.

.

"Wasaidizi Hawa ni Sehemu ya Mkakati Huu. Kampeni Hii ni ya Miaka 3 ambayo inatarajiwa Kukamilika February 2026 na Baada ya Hapo Tathmini Ya Kampeni Hiyo Itafanyika" Amesema Ndumbaro.

.

Waziri Huyo Amesema wanakwenda Kuhakikisha Kwamba wanyonge na Ambao hawawezi kumudu Gharama za Mawakili na Wana Sheria Mbalimbali wanakwenda kuipata hiyo.

.

Aidha, Ndumbaro Amesema Mkakati Wa Kampeni Hiyo unakuja Kugusa Malalamiko Ya Ukiukwaji Wa Maadili Na Uvunjifu Wa Sheria Ili Kuwapa Watanzania kile ambacho wanastahili Katika Haki Na Sheria.

#JordanMediupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn