SHIRIKA LA POSTA YATOA MADAWATI 100 NYANSHA MKOANI KIGOMA
Shirika la Posta Tanzania limetoa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Nyansha, Wilaya ya Kasulu mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi hivyo kutimiza ndoto zao, leo tarehe 23 Septemba, 2023.
Madawati hayo yaliyokabidhiwa kwa Mbunge wa Kasulu Mjini ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Prof.Joyce Ndalichako yamekuwa ni sehemu ya kuigusa jamii hasa katika sekta ya Elimu Wilayani humo.
Katika makabidhiano hayo Profesa Ndalichako ameeleza kuwa, kwa sasa Serikali ya Awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka vipaumbele katika huduma muhimu za jamii ikiwemo Sekta ya Elimu nchini ambapo elimu ndiyo msingi wa kulitoa taifa letu katika umaskini na kuwajengea uwezo wananchi katika kulikuza Taifa kichumi.
Aidha, Waziri Ndalichako ametumia nafasi hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Elimu nchini na kuchangia madawati hayo 100 kwa Shule ya Msingi Nyansha lengo ikiwa kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi kujifunza.
Akizungumza kwa niaba ya Postamasta Mkuu, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Bw.Amos Millinga ameeleza kuwa Shirika la Posta linatambua juhudi mbalimbali za Serikali zinazolenga kuboresha sekta ya elimu hivyo Shirika limeona liunge mkono kuboresha mazingira ya elimu kwa wananchi na wadau wa elimu.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

