WATANZANIA TUSHIRIKI KUPANDA MITI ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
MKURUGENZI wa Kampuni ya Ruthberta Supply inayojishughulisha na uzalishaji na uuzaji wa miche ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda Ruthberth Myonga amewaasa watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kikamilifu katika upandaji miti Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa leo Septemba 22 Mwaka huu Mkoani Geita na Mkurugenzi wa Ruthberth,Ruthberth Myonga kwenye Maonyesho ya 6 ya Teknolojia Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Bombambili.
.
Amewahamasisha wanawake kote nchini kupanda miti mbalimbali ya matunda na kivuli Kwa lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.
.
"Kupanda miti kuna umuhimu kumbwa sana ingawa siyo Kila mtu ni wa kupanda,hii inawezesha kusaidia Kuzuia majanga mbalimbali ,Kuna aina ya miti kama miharadani kama unataka kupanda miti hii usichukie popo angalia una faida gani kwa miaka 200 ijayo."amesema Myonga
Amesema kwa kutumia maonyesho hayo amekuja na miti ya matunda katika mkoa wa Geita kutokana na mkoa huo kukata mingi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji huku akisema miti hiyo itasaidia katika kuboresha Afya zao lakini pia kurudisha uoto wa asili.
Ametumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania kufuatilia vyombo vya habari Ili waweze kujifunza vitu mbalimbali katika maonyesho hayo ikiwemo shughuli za utunzaji mazingira.
Aidha,amesema mbali na kupanda miti ya matunda pia amewaasa wajikite katika kupanda miti ya maua ambayo pia ni fursa katika kujikwamua kiuchumi.
"Ruthberta Kampuni tupo katika Maonyesho haya lengo kubwa nikuja kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza na ikimbukwe kuwa hivi Sasa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni muhimu Kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayozunguka
"amesema na kuongeza kuwa
"Hivi sasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwemo Mkoa huu wa Geita kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kupanda miti ya matunda na hata hapa mmeona watu mbalimbali wanakuja kuuliza na kununua miti kwani wamejua umuhimu wa kupanda miti ."
Myonga ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau ikiwa pamoja na kutoa matamko mbalimbali yanayohamasisha upandaji wa miti .
"Kupitia Kampuni ya Ruthberta tutahakikisha tunaongeza kasi ya kuelimisha Watanzania pamoja na kuzalisha miti Kwa wingi ili kila Mwananchi apande miti Ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa katika suala Zima la utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ."amesema Myonga
Ameihakikishia Serikali na wananchi kwanunumla kuwa Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa mazingira ,itafuatilia ili kupata taarifa mbalimbali zinazohusu utunzaji wa mazingira kwa lengo la kupungaza kasi ya ukataji miti kitendo ambacho ni chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

