logo

WAZIRI UMMY: WATOTO ZAIDI YA MILIONI 3 KUPATA CHANJO YA POLIO MIKOA 6 NCHINI

Wizara ya Afya kwa kushirikiana Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau wa Sekta ya Afya inatarajia kuendesha Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto zaidi ya Milioni 3,250,598 walio chini ya miaka 8 kwenye Mkoa wa Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu leo Jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika nchini kuanzia Septemba 21 hadi 24, 2023.

.

Ummy amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwafikia watoto 3,250,598

waliozaliwa baada ya mwaka 2016 ili kuwakinga dhidi ya Kirusi cha

Polio aina ya pili(Polio Virus Type 2) kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu.

.

"Kwa Mkoa wa Rukwa tunatarajia kufikia watoto 391,883, Kagera

729,387, Kigoma 884,477, Mbeya 614,346, Katavi 227,862 na Songwe

402,643" amesema Ummy.

.

Amesema ili kufanikisha kampeni hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wadau wa chanjo imeshafanya maandalizi kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo kuendeshwa bila kuathiri shughuli zingine za wananchi.

.

"Timu hizi zitakuwa zinatoa huduma ya chanjo kwa walengwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya, nyumba kwa nyumba, shuleni na maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ikiwemo Nyumba za Ibada" amesema Waziri Ummy.

Waziri huyo ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara zitakazohusika na zoezi hilo kusimamia kwa karibu maandalizi na

utekelezaji wa kampeni hiyo kupitia Kamati za Afya ya Msingi ngazi za Mikoa na Wilaya.

.

Aidha,Ummy amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha upatikanaji wa chanjo, vifaa na mafunzo kwa wataalam watakaohusika katika utoaji wa chanjo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Tumaini Nagu amesema katika kuendeleza mikakati ya kutoa chanjo dhidi ya Polio, imeundwa timu ya watu waliopata mafunzo ya kutoa chanjo hiyo katika Mikoa hiyo sita.

“Tumeunda timu nzuri ambayo imepata mafunzo ya kutoa chanjo ambayo ina watoa huduma Elfu Tano Mia Mbili Tisini na Moja (5,291) katika Mikoa hiyo Sita ili kuhakikisha watoto wote wanafikiwa katika kupatiwa Chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio” amesema Nagu.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn