RAIS SAMIA: ILI KUPUNGUZA RUSHWA, TUNA MPANGO WA KUFUNGA CAMERA KATIKA BARABARA KUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema Ili kupunguza Rushwa Serikali ina mpango wa kufunga kamera katika barabara kuu ili kuondoa idadi kubwa ya Askari wa Usalama barabarani.
.
Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 04,2023 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Maafisa wakuu waandamizi wa Polisi katika Viwanja vya Polisi Officers Mess Oysterbay Jijini Dar Es Salaam.
.
Amesema anakwenda kutafuta bajeti ya Bilioni ya 125 iliyoombwa na IGP kwa ajili ya kusimamia vyema Uchaguzi wa 2024 na 2025 ili Jeshi la Polisi liweze kusimamia vyema Chaguzi hizo kwa kushirikiana na Majeshi mengine.
.
Aidha, Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na wananchi kupitia falsafa ya Polisi Jamii ili kuondoa uhalifu katika Jamii.
.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Masauni amesema kupitia Polisi Jamii uhalifu umepungua nchini na mradi wa Polisi Kata umesaidia sana ambapo Wakaguzi wa Polisi wamekuwa wakifanya kazi kubwa kwenye Kata zao.
.
Aidha, naye Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura amesema Jeshi la Polisi limeanza maandalizi kwa ajili kusimamia Uchaguzi kwa kuwajengea uwezo Maafisa wake na katika Mkutano huo watajadili na kuweka mikakati kwa ajili ya chaguzi zijazo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

