logo

MSANII HAITHAM KIM AFARIKI DUNIA HOSPITALI YA TEMEKE

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Haitham Kim amefariki Dunia mapema leo Septemba mosi wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Temeke Dar es Salaam

Taarifa za awali kutoka kwa ndugu wa karibu wa mwimbaji huyo ni kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mapafu.

Haitham Kim alifanya vizuri na kibao kama Playboy alichokitoa mwaka 2016 na kuendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo mbalimbali ikiwamo 'HAKUTAKI' aliyoiachia mwezi wa sita mwaka huu 2023.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn