MKURUGENZI MKUU WA UMOJA WA POSTA DUNIANI (UPU) AWASILI NCHINI TANZANIA
Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) Bw. Mesahiko Metoki amewasili nchini leo kwa ajili kushiriki uzinduzi wa Jengo jipya la Umoja wa Posta Afrika (PAPU).
Metoki ameambatana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) Bw. Mutua Muthusi pamoja na Aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa PAPU Bw.Younouss Djibrine.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Bw. Metoki amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Bi. Jessica Sengooba aliyeambatana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw.Macrice Mbodo.
Katika Msafara wa kumpokea Bw. Metoki pia alikuwepo Mtaalam wa Miradi wa Umoja wa Posta Duniani kwa ukanda wa Afrika Mashariki ambaye pia ni mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Bw.Tumaini Nguto.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

