MAVUNDE AWATAKA VIJANA KWENDA KUTUMIA UJUZI WAO VIZURI ILI WAWEZE KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde(MB) amewahimiza wahitimu wa mradi wa kukuza ajira kwa vijana nchini Tanzania (E4DT) kuwa na ujasiri na kujiamini katika kutumia ujuzi wao na kuanzisha miradi yao wenyewe.
.
Mavunde ameyasema hayo leo Agosti 24,2023 alipokuwa akifungua kongamano la Ujuzi na Ajira lililofanyika katika Viwanja Vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
.
Amesema uaminifu, uadilifu na bidii katika kazi ni vigezo muhimu sana katika mafanikio kwenye ajira ya kuajiriwa au kujiajiri.
.
"Tanzania ina fursa nyingi za ujasiriamali na mahitaji makubwa katika soko la ajira. Kupitia mafunzo haya, vijana mmepata ujuzi unaohitajika katika sekta mbalimbali za viwanda, ujenzi, na teknolojia. Hii ni fursa nzuri ya kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kujenga ajira kwa wengine" amesema Mavunde.
.
Naibu Waziri huyo amewataka vijana hao kwenda kutumia ujuzi wao vizuri na wakawe mabalozi wa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa kwenye Vyuo vya VETA nchini.
.
Kwa upande wa waajiri, Mavunde amewaomba waendelee kuwekeza kwa kuwatumia vijana wenye ujuzi kwa kuwapatia fursa za kazi na mafunzo ili waweze kuendeleza ujuzi wao na kuchangia katika ukuaji wa biashara zenu.
.
Aidha, Mavunde ametoa wito kwa wabia wa Maendeleo, na sekta binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa ajili ya kukuza ujuzi na ajira kwa vijana.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

