JWTZ YATOA SIKU SABA '7', WENYE SARE ZA KIJESHI WAZISALIMISHE HARAKA
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa wito kwa wananchi wote nchini kuyasalimisha mavazi yanayofanana na sare za kijeshi ndani ya siku saba (7) kuanzia leo Agosti 24 mpaka Agosti 30 mwaka huu 2023 na baada ya Siku Saba atakayekutwa nazo atachukuliwa hatua za kisheria.
.
Hayo yamesemwa leo Agosti 24,2023 na kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiano makao makuu ya Jeshi(JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius G. Ilonda alipokuwa akizungumza Na waandishi wa habari katika Ukumbi Wa Idara Ya Habari Maelezo Jijini Dodoma.
.
Luteni Kanali Ilonda amesema katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu Cha sheria 99 Cha sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
.
"Kifungu cha 178 cha sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16(Penal Code) na kifungu cha 6 cha sheria ya Usalama wa Taifa, vinakataza Raia kuvaa sare na Mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo" amesema Ilonda.
.
Aidha, Luteni Kanali Huyo amesema wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakiyatumia mavazi hayo kutapeli watu na wakidhani ni wanajeshi, vitendo hivyo ni uvunjifu wa sheria za nchi hivyo halipaswi kufumbiwa macho.
.
"Hali hii ikiachwa kuendelea inaweza kuhatarisha Ulinzi na Usalama Wa nchi yetu" amesema.
.
Kwa upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Ndg.Gerson Msigwa amewaomba wazazi kuwaelekeza watoto kutokuvaa mavazi hayo kama fasheni na waende wakawasimamie watoto hao majumbani.
.
"Vijana wanaona ni kama fasheni lakini wanavunja sheria kwahiyo wazazi ni vizuri tukalipokea tangazo hili kwa uzito wake na tukawasimamie Vijana wetu" amesema Msigwa.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news